BURUDANI Rosa Ree afunguka kuhusu Rayvanny na Bill Nass, ‘Mwanzo nilijua ataua’ (+video)
Rapper Rosa Ree amefunguka kuhusu verse ya Bill Nass kutolewa katika remix ya ngoma ya Rayvanny ‘Pochi Nene’\
Rapper huyo amesema kuwa anaamini kuondolea kwa verse ya Bill Nass ni kwa maana nzuri tu ingawa hawezi kulisemea sana.
“Kwanza mwanzo nilijua Bill Nass ataua lakini sijui ni kwanini baadaye hakuwepo lakini naamini wana sababu nzuri kwanini Bill Nass hayupo. Hivi vitu mara nyingi vinakuwa vya menejimenti, kwa hiyo siwezi nikavizungumzia mimi msanii ambaye sihusiki na menejimenti za hawa watu wawili,” Rosa Ree ameiambia Bongo5.
Rosa Ree ndiye msanii pekee wa kike aliyesikika katika remix ya ngoma hiyo, wasanii wengine ni pamoja na Khaligraph Jones, Godzilla, Rosa Ree, Izzo Bizness, Country Boy, Young Dee na Wakorinto.

Post a Comment