Header Ads

BURUDANI Nyimbo mbili anazozikubali Ommy Dimpoz kutoka WCB

Msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz ametaja nyimbo mbili kutoka label ya WCB ambazo anaona zinafanya vizuri.
Mumbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Wanje’ ametaja ngoma ngoma hizo kuwa ni Kwa Ngwaru ya Harmonize na Pochi Nene ya Rayvanny.

“Moja wapo ni hiyo kama unavyosema Kwa Ngwaru ni wimbo ambao unafanya vizuri, yeah!, kuna mwingine nimesikia wa Rayvanny Pochi Nene, kwa hiyo kwa currently ni nyimbo ambazo naweza kusema zinafanya vizuri,” Dimpoz ameiambia Citizen Radio.
Katika hatua nyingine amefunguka ni lini hasa bifu lake na Diamond litaisha kwa kusema; “Kila jambo lina wakati wake kwa hiyo time itakapofika mambo yote yatakaa sawa, tuombe Mungu’.

No comments