Orodha ya vijana 100 wenye ushawishi zaidi barani Afrika yatajwa, Tanzania yatoa vijana 8 ‘Diamond na Jokate watoswa’
Taasisi inayojishughulisha na tafiti mbalimbali zinazohusu vijana wenye ushawishi zaidi walio chini ya miaka 40 barani Afrika ya The Africa Youth Awards, imetangaza orodha ya majina ya vijana 100 ya vijana wenye ushawishi kutoka kwenye mataifa 26 barani Afrika kwa mwaka 2018, na Tanzania ikiwemo.

Kutoka Tanzania, vijana waliofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo ni vijana 8 ambapo majina hayo ni Alikiba, Faraja Nyalandu, Herieth Paul, Jennifer Bash, Jumanne Mtambalike, Mbwana Samatta, Millard Ayo na Yusuf Bakhresa.
Kwa upande majina makubwa ambayo mwaka jana 2017 yalitangazwa kwenye orodha hiyo kama, Diamond Platnumz, Idris Sultan na Flaviana Matata mwaka huu yamepigwa chini.
Tazama orodha kamili hapa chini na kusoma zaidi kwenye website ya The Africa Youth Awards.

Post a Comment