Header Ads

Vitu sita ambavyo simu yako inaweza kufanya na pengine hukujua

Vitu sita ambavyo simu yako inaweza kufanya na pengine hukujua

Simu yako ya rununu ina matumizi mengine zaidi ya kusoma ujumbe wa WhatsAp pekee


Je unatumia simu yako kufanyia nini?

Mbali na kuandika ujumbe wa WhatsApp , kupiga simu kuangalia mtandao wa facebook na Instagram kuona kile rafiki zako walichochapisha, simu yako ya rununu inaweza kukusaidia zaidi.
Tunakueleza matumizi mengine ya simu yako ambayo hukuyajua

1.Unaweza kupiga picha huku ukirekodi kanda za video

Upigaji picha wa simu umekuwa jambo la kila siku kutokana na uwepo wa mtandao na mitandao ya kijamii

Kila siku mamilioni ya raia huchukua na hata kusambaza picha kwa kutumia simu zao za rununu. Kanda fupi za video pia zimesheni.

Lakini je unajua kwamba unaweza kupiga picha wakati unapoendelea kurekodi kanda ya video?
Unaweza kwa kutumia simu aina ya Adroid pamoja na ile ya iPhone.
je unataka kupiga picha ukirekodi?

Kwanza gusa skrini yako unaporekodi video , iwapo una simu aina ya iPhone unatakiwa kubonyeza mahali unapotumia kupiga picha , kitufe cheupe karibu na kitufe cha kurekodi video.



Iwapo una iPhone bonyeza na kuzuia kitufe cheupe kushoto mwa kitufe chekundu cha kurekodia unaporekodi
Hatahivyo hali ya picha hizo haiwezi kuwa nzuri ukilinganisha na ile ambayo unapeta iwapo ungekuwa unapiga picha picha ya kawaida , lakini ni njia mojawapo ya kupiga picha kitu kinachofanyika wakati huo.

2.Unaweza kusoma ujumbe wako na emoji

Je umechoka kutazama skrini ya simu yako mara kwa mara?
Unaweza kutumia simu yako kusoma ujumbe unaopokea kana kwamba unasikiza redio.
Cha kufanya, sema neno hili kwa simu yako: Siri- au Google iwapo unatumia simu aina ya Adroid- soma ujumbe wangu.
Halafu unaweza kuamua iwapo utazijibu ama iwapo unataka simu yako aina ya smartphone kurudia tena ujumbe huo.
Ujanja huo sio tu kwa ujumbe wa SMS: Pia unaweza kuutumia kwa WhatsApp.
Je wajua kwamba siku yako inaweza kusoma emoji?



 Iwapo una simu aina ya Apple, ambia Siri. ''Siri nisomeee ujumbe mpya wa WhatsApp''. Itausoma mara moja. Pia itakwambia ni nani aliyetuma na ni wakati gani uliwasili. lakini la kufurahisha ni vile inavyosoma emoji. jaribu!.
Iwapo unatumia simu aina ya Adroid , ni sharti utumie programu fulani. Programu hizo ni Hatomic ama ReadItToMe

3.Wazuie wengine kutotumia programu ya simu yako

Iwapo utamsaidia rafiki yako kwa kumpatia simu yako lakini hutaki afungue programu zako ama kusoma ujumbe wako wa WhatsApp unaweza kubadili programu zako na kumzuia na kutoweza kuingia bila kutumia neno la siri.
Unaweza kutumia programu mbadala kwa jina 'Guided Aces's katika setting na baadaye nenda kwa accesibility na kubonyeza kitufe cha programu hiyo unayotaka kubadilisha .
Iwapo ni Android utaipata katika location na security.



Unaweza kuzuia matumizi ya programu nyengine
Pia unaweza kutumia programu kama vile Applock ambayo pia inazuia mtu kuingia katika programu ya Google play ili asiweze kupakua programu bila wewe kujua.
Programu nyengine mbadala ni ile ya Hexlock ambayo inakuwezesha kutengeneza 'profile' tofauti za watu na imeelezewa iwapo unataka kuwaachia watoto simu yako.
Iwapo una simu aina ya Iphone , tumia programu ya Notes.
Katika kitufe cha alama ya ongeza tumia Scan documents. Hatua nyengine unazofaa kuchukua ziko sawa kama zile zinazotumika na Google drive., mwisho bonyeza kitufe cha hifadhi ama save.

4.Kusawazisha

Iwapo unataka kuweka boksi katika eneo tambarare lenye usawa unaweza kutumia simu yako
Katika iOs kuna kitufe mbadala kilichojificha kwa jina Measure programu



kipimo cha kusawazisha kipo ndani ya simu yako ya iphone

5. Kutambua vyuma

Iwapo umepoteza pete yako ama vipuli vyako vya dhahabu na huwezi kuvipata simu yako inaweza kuwa kifaa muhimu sana
Kwa wale wanaotumia simu aina ya Android , kuna programu inayotoa fursa hiyo kwa jina Metal Detector.
Ni bure na inatumia sensa ya sumaku ya simu yako.
Matumizi yake ni rahisi sana: Fungua programu hiyo , peleka simu hiyo mahali unapotafuta kifaa hicho cha chuma , iwapo una bahati simu hiyo itapiga king'ora.



je umepoteza pete yako?, tumia simu yako kuitafuta
6. Kuskani Nyaraka
Iwapo una nyaraka ambayo unahitaji kwenda katika tarakilishi lakini hauna skana , unaweza kutumia simu yako ya rununu.
Kupitia programu kama vile Genius scan , Cam Scanner na Office Lens unaweza kubadilisha nyaraka yoyote kidijali kwa sekunde chache.
Unaweza kufungua programu ya Google Drive katika simu aina ya Android ambayo iko huru -ongeza kitufe (the + symbol) chagua kitufe kilichoandikwa "Scanning" ili kuamsha kamera ya simu yako.
Kuskani nyaraka kwa kutumia simu yako ni rahisi mno.
Unapoipima vizuri na kuhakikisha kuwa nyaraka zote zipo ndani ya skrini chukua nyaraka hizo na kuweka ndani ya picha . Kwa kubonyeza kitufe cha Accept picha hiyo itahifadhiwa katika PDF.








No comments