Header Ads

Hapa ndio mahali atakapozikwa Dkt Mengi, familia yaitaja siku ya kuwasili mwili wake (+ Video)

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi utawasili jumatatu mchana Mei 6, 2019 jijini Dar es salaam kutoka Dubai ambapo alifikwa na umauti jumatano usiku. Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo amesema mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu nchini Tanzania utahifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo baada ya kuwasili. Siku ya Jumanne,marehemu ataagwa katika viwanja vya Karimjee.siku ya Jumatano Mei 8, 2019 mwili utasafirishwa kwenda Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika siku ya Alhamisi Mei 9, 2019. “Baada ya mwili kuwasili Machame ibada ya mazishi itafanyika katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania la Kisereni,”








Ikumbukwe mzee Mengi alizaliwa mwaka 1942 mkoani Kilimanjaro na umauti umemkuta akiwa mjini Dubai, Falme za Kiarabu baada ya kuugua kwa muda mfupi, kwa mujibu wa familia yake.

Umauti umemfika akiwa na umri wa miaka 77, huku akicha mke na watoo wanne.

No comments