Jinsi ya Kutambua kama Memori kadi (SD Card) ni feki au la!
Jinsi ya Kutambua kama Memori kadi (SD Card) ni feki au la! #kwa msaada wasiliana na sowetocb ICT ltd. tel 》0738283964
Umekwisha nunua memori kadi (SD Card) ya GB 4, 8 n.k kisha muda wa kuitumia unagundua ni nusu ya ujazo huo uliokua umeandikwa kwenye kadi? Au data zinakuwa zinapotea mara kwa mara…Basi ujue umenunua SD Card feki.
Wengi huwa wanajikuta wanatumia pesa zaidi wakijua wanapata memori kadi ya ukubwa unaoonekana juu ya kadi hizo lakini mwisho wa siku ni utapeli tuu.
Tunashukuru walioulizia juu ya jambo hili na leo tutakufundisha njia kadhaa za kuzitambua kama ni orijino au feki.
> KABLA YA KUNUNUA
Fahamu aina za Memori kadi (SD Card)
Kuna aina kuu tatu. Hapa cha muhimu kujua ni kuzifahamu hizi alama zake, ukikuta memori kadi imeandikwa ina ukubwa wa GB 8 na huku ukiiangalia haina alama ya familia hiyo basi utambue unanunua kimeo.
Fahamu tofauti za muonekano wa logo na majina yake, SDSC(SD), SDHC na SDXC…pia kiasi cha ukubwa unaotegemewa kwa aina hiyo ya memori kadi. Ukiona tu haviendani ujue unanunua bomu. Kuna viwanda vingi bubu vinavyotengeneza memori kadi na kuiga majina ya makampuni makubwa lakini huwa hizo logo wanaweka ovyo ovyo tuu.
Post a Comment