Matokeo ya uchaguzi DRC
Felix Tshisekedi
Matokeo ya awali yameonyesha kuwa yeye anaongoza katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya mgombea wa upinzani Martin Fayulu, na yule wa muungano wa chama tawala Emmanuel Shadary.
Mapema majira ya alfajiri Alhamisi mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi DRC (CENI), Corneille Nangaa, ametangaza Tshisekedi “alipata kura asilimia 38.57”.
Atakapo thibitishwa, Tshisekedi atakuwa mshindani mpinzani wa kwanza kushinda tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupata uhuru.
Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya miaka 18 ya uongozi wake.
Alikuwa ameahidi kuwepo kubadilishana madaraka kwa njia ya utulivu DRC tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Ubelgiji 1960.
Post a Comment